
Ameyasema hayo
mapema leo mjini Dodoma wakati akifungua
mkutano wa 25 wa baraza la wafanyakazi wa
wizara ya Maliasili na Utalii ambapo amesema kuwa serikali haitosita kuchukua hatua kali kwa
watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Waziri Kigwangala amesema
hivi karibun kumekuwepo na taarifa za ujangili ,usafirishaji haramu wa magogo
na wanyama pori vinavyofanywa na wananchi wasio na uzalendo kwa kushirikiana na
baadhi ya watumishi wa wizara jambo ambalo limekuwa likiipotezea serikali mapato
hivyo kusaababisha kurudisha nyuma jitihada za kuimarisha uchumi wa Taifa.
Akizungumzia
mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa wizara kwa kipindi tofauti Dkt
Kigwangala amesema kuwa matukio ya ujangili,biashara haramu ya rasilimali za
misitu na wanayama pori yamepungua kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na
kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka milioni 1,284,279 mwaka 2016 hadi
kufikia milioni 1,327,143 kwa mwaka 2017.
Awali akisoma
taarifa ya wizara kwa waziri Kigwangala katibu mkuu wizara ya maliaslili na
utalii meja Jenerali Gaudience Milanzi amesema kuwa tayari wizara imekwisha
kuanza mchakato wa kuazisha jeshi
maalumu litakalosimamia rasilimali zote katika maeneo yote ya hifandhi nchini
na amewasihi watumishi wote kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kufikia
malengo.
NA
ALFRED BULAHYA DODOMA
FM
Comments
Post a Comment