Uongozi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kongwa wanatarajia kuigawanya shule ya msingi Ibwaga mara tu
zitakapopatikana fedha za kufanikisha ujenzi huo kutokana na wingi wa wanafunzi
katika shule hiyo pamoja na wale wanaoendelea kuandikishwa.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Halshauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Ngusa Izengo ameyasema hayo wakati
akiongea na kituo hiki kwa njia ya simu ikiwa ni siku chache baada ya kituo
hiki kufika katika shule ya msingi Ibwaga na kujionea changamoto ya upungu wa
matundu ya vyoo.
Amesema kutokana na
shule hiyo kuwa na eneo kubwa la kutosha hivyo wanafikiria kuanzisha shule
nyingine ili kupunguza msongamano wa watoto katika shule hiyo ambayo
inakadiriwa kufikia idadi ya wanafunzi 1000 huku ikikabiliwa na upungufu wa
matundu ya vyoo yapatayo 41.
Amesema changamoto
hiyo inatarajiwa kutatuliwa ndani ya mwezi wa tatu mwaka huu kutokana na
jitihada zinazoendelea kuchukuliwa huku mkakati mkubwa ikiwa ni kuigawanya
shule hiyo ili kuondoa msongamano wa wanafunzi.
Mwishoni mwa wiki
iliyopita kituo hiki kilitembelea katika shule ya msingi Ibwaga WilayanI Kongwa
na kuzungumza na makamu mkuu wa shule hiyo Mwalimu Edefrida Mzeru ambapo
alibainisha wazi kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo 49 lakini
yaliyopo kwa sasa ni matundu 10 pekee.
Na
Pius Jayunga
Dodoma FM
Comments
Post a Comment