Halmashauri ya wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma imejipanga kuondoa utoro mashuleni kwa kuwapatia wanafunzi chakula cha mchana.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wilaya ya
Kongwa Bwana Adifasi Mushi alipokuwa akizungumza na Dodoma FM kwa niaba ya Mkuu
wa Wilaya juu ya namna ambavyo wamejipanga kudhibiti utoro.
Bwana Mushi amesema serikali inaendelea kushirikiana na
wananchi kuhakikisha chakula kinapatikana mashuleni.
Aidha Bwana Mushi amewakumbusha wananchi
kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mazao ya biashara na chakula ili kiwasaidie kuwawezesha watoto wao kuwa na
chakula cha kutosha shuleni.
Kwa upande mwingine amewataka wakuu wa shule kuwawajibisha baadhi
wa watumishi wanaofanya kazi kinyume na maadili ya kazi yao, kwani wao ni
msingi na kioo katika jamii inayowazunguka.
Na Victor Makwawa Dodoma
FM
Comments
Post a Comment