Waziri
wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof Makame Mbarawa amesema serikali
haitasita kumchukulia hatua mtumishi yeyote atakayeonekana kuwa chanzo cha
kukwamisha malengo ya bajeti wakati wa kufanya mapitio ya bajeti ya nusu mwaka
hapo baadae.
kauli hiyo imetolewa
leo na Eng. Joseph Nyamhanga alipokuwa akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa
ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof Makame Mbarawa wakati wa kufungua mkutano
wa baraza la wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi mjini Dodoma.
Amesema kuwa
serikali itakapokuwa ikifanya mapitio ya bajeti ya nusu mwaka hapo baadae na
kugundua uwepo ukiukwaji wa taratibu zilizowekwa haitosita kumwajibisha
mtumishi yeyote atakayeonekana kutotimiza malengo ya bajeti hiyo hivyo ni vyema
watumishi wakazingatia maelekezo ili kila mmoja atekeleze majukumu yake
ipasavyo.
Hata hivyo ameitaka
menejimenti ya wizara na chama cha wafanyakazi TUGHE kuhakikisha kuwa zinafanya
kazi kwa mshikamano thabiti katika kufikia maamuzi mbalimbali ya kisera na
kitaaluma ambayo yatafanikisha shughuli za sekta ya uchukuzi na tabiri za hali
ya hewa kufikia malengo yao.
Awali akisoma
taarifa ya baraza la wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi mwenyekiti wa baraza la
wafanyakazi la wizara ya uchukuzi dkt Leonard Chamriho amesema kuwa sekta ya
uchukuzi kwa mwaka mpya wa fedha unaokuja 2017/18 imejiwekea malengo ya
kuboresha miundombinu ya hali ya hewa, ununuzi wa ndege mpya 4 kwa ajili ya
kuboresha huduma za ATCL pamoja na kutekeleza awamu ya pili na ya tatu ya
serikali kuhamia Dodoma.
Na Alfred Bulahya
DODOMA FM
Comments
Post a Comment