Katibu wa baraza la
taifa la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi manispaa ya Dodoma ENOCK ANDREA
amewahimiza Wazazi kuzingatia kuwapima watoto wao na kufahamu afya zao ili
kuwalinda na kuwaweka katika mazingira salama.
Akizungumza na
Dodoma FM kupitia kipindi cha Taswira ya habari amesema kuwa mwitikio wa wazazi katika kupima virusi vya ukimwi
hauridhishi kwani wengi wao hawajiamini na kupelekea kushindwa kuwapeleka
watoto wao kwenye vituo vya afya ili kutambua afya zao.
Katika hatua
nyingine ameongeza kuwa kuna watoto ambao wanazaliwa na maambukizi ya virusi
vya ukimwi hivyo kuwapeleka watoto mapema kupimwa afya zao ina rahisisha
kuwatambua na kuwapa uangalizi mzuri
Kwa upande wake
kaimu mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi mkoani hapa
DORAH MWAUKO ameongeza kuwa wamekuwa na utaratibu wa kuwahamasisha wazazi kwa
kuwapatia elimu ya umuhimu wa upimaji afya za watoto ili kuwakinga na
maambukizi.
Baadhi ya wazazi
wamekili kuwa kuna kasumba ya baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwalea watoto
wao pasipo kujua afya zao na hivyo kusababisha watoto wao kutokuwa na mazoea ya
kwenda kupima afya zao wanapokuwa watu wazima.
Na,Mindi
Joseph
Dodoma Fm
Comments
Post a Comment