Imeelezwa kuwa
ongezeko la watoto wanaoishi mitaani
linatokana na baadhi ya wazazi na walezi kuwafukuza majumbani na kutowafuatilia.
Hayo yamesemwa na baadhi
ya wazazi na walezi wakati wakizungumza na Dodoma FM kwa nyakati tofauti katika manispaa ya Dodoma ambapo wamesema kuwa
mazingira ya malezi kwa watoto hao ndiyo huwafanya kukimbilia mjini na kuiomba
serikali kutenga shule kwa ajili ya watoto hao wawapo mijini.
Wazazi hao wamesema
wapo watoto wengine ambao urudishwa nyumbani lakini muda mchache hurejea mjini
chanzo kikiwa ni malezi duni na
ufatiliaji mdogo wa wazazi kukosa kwenda shule huku wengine kukutwa na ile hali
ya kuuzoea mji jambo ambalo uongeza idadi kubwa ya watoto waishio mitaani.
Kauli hiyo inakuja
siku chache baada ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma GILLES MURUTO
kuwataka wazazi na walezi kuwafatilia watoto wao kupitia mkutano alioufanya na
wanahabari na kusema kuwa kutofanya hivyo huwapelekea watoto hao baadaye kuwa
wahalifu.
Na
Rweikiza Katebalirwe Dodomafm
Comments
Post a Comment