Katibu
mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dk.Florence Tuluka
amewataka watumishi nchini kujiunga na vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) ili
kupata nafuu ya maisha watakapostaafu.
Katika ufunguzi wa semina ya wakuu wa
vyuo,shule na makamanda wa vikosi iliyofanyika mkoani Dodoma Dr Florence
amesema kila mtumishi ana wajibu wa
kujiwekea akiba pia kukopa katika saccos kutokana na riba nafuu zinazotolewa
ambazo zipo tofauti na maeneo mengine wanayokopesha.
Aidha amesema Pamoja na elimu ya
ushirika na ujasiliamali inayotolewa lakini kila mmoja ana wajibu wa kujiunga
na Ngome Saccos ili kujiwekea akiba na kupata mikopo kwa kuwa mtumishi yeyote
ni mstaafu mtarajiwa.
Tuluka ameongeza kuwa semina
wanayoifanya itawawezesha kufahamu utendaji kazi wa SACCOS pia
itawashawishi wakuu ambao hawajajiunga na chama hicho cha kuweka na kukopa
waweze kujiunga.
Hata hivyo amesema elimu ya
ushirika ambayo itatolewa ina umuhimu wa kipekee katika kuujenga ushirika imara
na itawaongoza katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
NGOME SACCOS ilipata
usajili mwaka 1967 na kuanza kutumika mwaka 2007 ikiwa na lengo la kutoa
mikopo ya dharura, mikopo ya maendeleo na mikopo ya wastaafu.
Mariam Matundu Dodoma FM
Comments
Post a Comment