Jeshi la Polisi
Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa kosa la matumzi mabaya ya
mitandao ya kijamii kwa kuhamasisha maandamano haramu yaliyopangwa kufanyika Nchini
tarehe 26 Aprili mwaka huu.
Kamanda wa jeshi la
polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi
wa habari mjini Dodoma na kueleza kuwa vijana hao wamebainika kusambaza taarifa
za kuhamasisha maandamano ya nchi nzima yenye viashiria vya uchochezi dhidi ya
Serikali na kutishia usalama wa nchi.
Amewataja
waliokamatwa kuwa ni pamoja na Amandus Manchali mwenye umri wa mika 31ambae ni
dereva wa shirika la bima ya afya NHIF pamoja na kijana Yuda Mbata mwenye umri
wa miaka 29 mkazi wa Kijiji cha mpamatwa Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.
Kamanda Muroto
amesema maandamano hayo yanayohamasishwa msingi wake ni kusababisha uhalifu,
kuhatarisha amani ya nchi, kuhatarisha usalama wa raia na mali zao na kutoa
wito kwa wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii badala
yake mitandao hiyo itumike kuchochea na kuharakisha maendeleo.
Baadhi ya wakazi wa
Manispaa ya Dodoma wakizungumza na kituo hiki wamesema bado elimu juu ya
matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii inapaswa kuendelea kutolewa ili wananchi
waweze kunufaika na uwepo wa mitandao hiyo badala ya kuitumia katika matumizi
yasiyokuwa sahihi.
Katika hatua
nyingine Kamanda Muroto amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani
Dodoma zimesababisha vifo vya watu watatu wote wa familia moja katika Kijiji
cha Gwandi Wilaya ya Chemba na kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari
mapema ikiwemo kuto kuvuka mito iliyo jaa maji.
Na
Pius Jayunga DODOMA
FM
Comments
Post a Comment