Jumla ya watu 200 hadi 225 wanapata maambukizi mapya ya virusi
vya ukimwi kwa siku ambapo asilimia 40 kati yao ni vijana wenye umri kati ya
miaka 15-24 na kati ya hao vijana jumla ya asilimia 80 ni vijana wa kike.
Takwimu hizo pia zimo katika ripoti ya tathimini ya mazingira ya kisheria
katika mwitikio wa ukimwi iliyozinduliwa desemba mosi mwaka jana katika siku ya
ukimwi duniani
Akielezea matokeo ya utafiti huo mjini dodoma mkurugenzi
mtendaji wa tume ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS) Dk.Leonard Maboko wakati
wa kikao cha siku mbili kwa ajili ya usambazaji wa ripoti hiyo ameeleza kuwa
jumla ya watu elfu 81 wanapata maambukizi mapya kwa mwaka ambayo ni sawa na
wastani wa watu 225 kwa siku.
Dr Maboko amesema katika tafiti zilizofanywa kwa mwaka 2016/17
zinaonyesha asilimia 91 ya waathirika wanaojua hali zao wamekwisha anza dawa na
asilimia 88 kati yao wamekwisha fubaza virusi vya ukimwi jambo
ambalo lipo katika hatua nzuri huku akiongeza kuwa wanaume ndio wanaoongoza
kwa kutopima VVU.
kwa upande wake mkurugenzi wa ufatiliaji na tathimini (TACAIDS ) Jerome Kamwela
amesema asilimia 80 ya maambulkizi ya ukimwi tanzania yanatokana na mahusiano
ya kingono na waliosalia hupata maambukizi kwa njia nyinginezo ambapo pia
ameelezea idadi ya watanzania wanaoishi na virusi vya ukimwi hadi hivi sasa.
Na Mariam Matundu Dodoma
FM
Comments
Post a Comment