Wanawake mjini Dodoma
wametakiwa kujituma kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili
kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano yenye lengo la kuwa na serikali
yenye uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo
imetolewa leo ma mbunge wa viti maalum mjini Dodoma Mh Fatuma Toufiq wakati
akitoa hotuba katika kilele cha maadhimisho ya wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa
katika viwanja vya kata ya Msalato Mjini Dodoma.
Mh Toufiq amesema
kuwa taifa linakabiliwa na chanagamoto
nyingi hivyo ni vyema wanawake wote wakaacha tabia ya kuwa wasindikizaji bali
wawe watendaji hali ambayo itawasaidia kufikia malengo kwa pamoja katika uchumi wa viwanda.
KATIKA hatua
nyingine Toufiq amezindua mpango kazi wa miaka 3 utakaosimamia jukwaa la
uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili hali
itakayowasaidia kuendeleza na kukuza ujasiria mali pamoja na biashara zao.
Awali akisoma risala
mratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi kutoka manispaa ya Dodoma Bi
Hidaya Mizega amesema kuwa wanawake wanapaswa kuzitambua fursa zilizopo na
kuzitumia.
Maadhimisho ya
wanawake duniani huadhimisha kila mwaka ifikapo machi 8 na kwa mwaka huu mkoani
Dodoma yameadhimishwa katika kata ya Msalato huku yakiwa yamebebwa na kauli mbiu
isemayo kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia kwa wanawake
vijijini.
Na
Alfred Bulahya Dodoma FM
Comments
Post a Comment