Magonjwa ya figo yanakadiriwa
kuwaathiri takribani wanawake milioni 195 duniani kote na yanashika nafasi ya 8
.
Chanzo cha vifo vya wanawake
duniai na inakadiriwa kuwa wanawake laki 6
hupoteza maisha kutokana na matatizo ya figo duniani kote kila mwaka.
Naibu waziri wa
afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dk. Faustine Ndugulile ameyasema
hayo wakati akitoa tamko la siku ya figo Duniani na kusema tafiti zilizofanywa
na shirika la afya Duniani (WHO) zinaonyesha wanawake wako katika hatari zaidi
ya kupata matatizo ya figo ikilinganishwa na wanaume kwa wastani wa 14% ya
wanawake wanaathiriwa na matatizo ya figo ikilinganishwa na asilimia 12 kwa
wanaume.
Amesema utafiti
uliofanywa na hospitali ya kanda ya Bugando umeonesha kuwa 83% ya wagonjwa wa
kisukari wana matatizo sugu ya figo na kati yao 25% wanahitaji huduma za
usafishaji damu huku mgonjwa mmoja akigharimu fedha kiasi cha sh. Mil. 37 kwa wastani wa safari 126 kwa mwaka.
Pamoja na hayo Dr.
Faustine ametoa wito kwa wananchi kubadili jinsi ya kuandaa chakula majumbani
kwa kupunguza kiasi cha chumvi katika chakula na kiasi cha mafuta ili kupunguza
ugonjwa wa shinikizo la damu kisukari na unene uliopitiliza na kuhamasisha
familia kujenga mazoea ya kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara.
Kwa upande wake
Rais wa chama cha madaktari bingwa wa figo Nchini Dr. Onesmo Kisanga amesema
lengo la chama cha madaktari wa figo hapa Nchini ni kuelimisha wananchi juu ya
umuhimu wa afya ya figo na ikiwemo swala la upimaji wa figo na tatizo la
ugonjwa huo likitajwa kusababishwa na magonjwa nyemelezi kama ugonjwa wa moyo
na kisukari hususani kwa upande wa kina
mama.
Maadhimisho ya siku
ya figo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 mwezi march na mwaka 2018 maadhimisho
hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo figo na afya ya wanawake: washirikishwe,
wathaminiwe na wawezeshwe.
Na
Pius Jayunga
Dodoma FM
Hakika tunapaswa kuchukua tahadhari kwa kupima afya zetu mara kwa mara.
ReplyDelete