
Wanaume mkoani
Dodoma wameshauriwa kuwa na desturi ya kutoa taarifa katika vyombo
vinavyosimamia masuala ya ukatili, pindi wanapofanyiwa ukatili ili kuendelea
kutokomeza ukatili katika jamii.
Kauli hiyo
imetolewa leo na mwanasheria kutoka katika taasisi ya sheria ya DARWINS ATORNEY AND CONSULTANTS ya
mjini Dodoma bw Chrispin Nicholaus Rwila wakati akizungumza na kituo hiki
ofisin kwake.
Amesema kuwa
wanaume wengi wamekuwa hawana desturi ya kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi
wanapofanyiwa ukatili, kutokana na kuogopa fedheha jambo ambalo linaweza
kusababisha madhara makubwa kama msongo wa mawazo na hata kifo.
Akizungumzia sheria
inayosimamia suala la ubakaji amesema kuwa sheria hiyo haijaweka wazi namna ya
kuwasaidia wanaume pindi wanapokumbwa na tatizo hilo, ambapo ameiomba serikali
kulitazama jambo hilo kwa jicho la tatu ili kuweka usawa kwa wananchi wote.
Nao baadhi ya
wakazi wa mji wa Dodoma wameiambia Dodoma Fm kuwa suala la wanaume kutotoa
taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili, linatokana na baadhi yao kuona aibu
kutokana na kujijengea mazingira ya kuamini kuwa mwanaume ndiyo kichwa cha familia, hivyo akionekana anatoa taarifa za kufanyiwa ukatili anaweza
kufedheheka.
Na Alfred Bulahya
DODOMA FM
Comments
Post a Comment