Wananchi wameiomba mamlaka ya
chakula na dawa TFDA kuchukua hatua kwa kufanya ukagunzi wa mara kwa mara kwa
wafanyabiashara pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa Jamii.
Hayo yamesemwa na
baadhi ya wanachi wakati wakizungumza na Dodoma FM ambapo wamebainisha kuwa baadhi ya bidhaa kama
vile unga,maharage pamoja na mchele huuzwa bila kuwa na tarehe ya kutengenezwa
pamoja na muda wa kuisha matumizi yake.
Wamesema imekuwa ni
changamoto ambayo inapelekea kununua bidhaa hizo zikiwa zimeharibika kutokana
na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kufanya ukanguzi mara chache kwa
wafanyabiashara.
Kwa upande
wake Meneja wa mamlaka ya chakula na
dawa TFDA kanda ya kati ENGLIBERT BILASHOBOKA amewataka wasindikaji kufuata
sheria ikiwa ni pamoja na kuweka tarehe ya kutengenezwa pamaoja na muda wa
kuisha kwa matumizi yake .
Dr Englibert ameongeza
kuwa elimu ya matumizi ya bidhaa inaendelea kutolewa kwa wanachi na wameelekeza
hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuhakikisha wanapotumia
bidhaa wanaangalia kwanza kwa ajili ya kulinda afya zao .
Na
Mindi Joseph
Dodoma Fm
Comments
Post a Comment