
Wadau wa maendeleo mkoani Dodoma wameshauriwa
kujenga desturi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili
kuendelea kuzitambua fursa zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika kukuza
uchumi wa nchi kupitia nyanja tofauti.
Ushauri huo
umetolewa na mratibu wa programu za utoaji taarifa kutoka katika Mtandao wa
Asasi za kiraia mkoani Dodoma NGONEDO Bwana Edward Mbogo wakati akizungumza na
Dodoma FM .
Bwana Mbogo
amesema kuwa ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi ni lazima kila mdau na mwananchi
kushiriki kikamilifu katika maendeleo mbalimbali kupitia mikutano ya
kimfumo,kutoka katika ngazi za vitongoji vijiji na kata ili kubaini fursa
mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kimaisha.
Aidha
ameitaka jamii mjini Dodoma kujijengea tabia
ya kuhudhuria katika mikutao ili kuleta maendeleo chanya na kuachana na
tabia ya kutohudhuria kwenye vikao mbalimbali ili kuongeza uwazi na uwajibika
katika kazi.
NGO NETWORK FOR DODOMA REGION (NGONEDO)
ni taasisi iliyoanzishwa mkoani Dodoma mnamo mwaka 2000 kwa lengo la kuwezesha
maendeleo jumuishi kwa jamii ili kujenga uwezo wa kuimarisha haki za
binadamu,utawala bora, kubadilishana uzoefu wa taarifa pamoja na kuratibu shughuli mbalimbali za
maendeleo.
Na Alfred
Bulahya DODOMA
FM
Comments
Post a Comment