Kuto kuwa na uelewa juu ya
masuala ya umiliki wa ardhi kwa baadhi ya wakazi nchini umetajwa kuwa ni sababu
mojawapo inayosababisha migogoro ya
ardhi katik.
Hayo yameelezwa na mwanasheria
na wakili wa kujitegemea Bwana Saidy Kamsumbile alipokuwa akizungumza na Dodoma
FM ambapo amebainisha kuwa tatizo la
migogoro ya ardhi ni la muda mrefu isipokuwa kuna baadhi ya wananchi hawana
uelewa juu ya sheria za umiliki ardhi.
Bwana Kamsumbile
amesema sheria hizo ni muhimu kwa wanachi wakazitambua kwa sababu wakazi wengi
hukumbwa na sintofahamu pale wanapo kumbwa na migogogoro ya ardhi na hatimaye
kushindwa kujua kama anahaki ya kushinda kesi mahakamani au kushindwa.
Pamoja na hayo
amesema kuna baadhi ya wananchi wanajitahidi kutembelea katika ofisi mbalimbali
za wanasheria kwa lengo la kutaka kujua sheria juu ya umiliki wa ardhi lakini
wanalazimika kutoa pesa ndipo wapatiwe elimu hiyo kitu ambacho sio haki.
Sanjari na hayo
amewataka wananchi kuwa makini pindi wanaponunua ardhi ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha eneo ambalo unanunua limepimwa na mamlaka husika ili kuepusha
migogoro.
Miongoni mwa wakazi
mkoani hapa akiwepo bwana Issa Rajabu amesema kuna umuhimu kwa kila mwananchi
kujua sheria angalau hata kidogo ili kusaidia kujitetea pindi upatapwo na
matatizo.
Kila mwaka wizara
ya katiba na sheria wadau wa maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayojihusisha na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria nchini huadhimisha
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria lengo kubwa ni kutoa elimu kwa umma
pamoja na watu mbalimbali waliopo polisi na gerezani.
Na
Benard Filbert
Dodoma FM
Comments
Post a Comment