Chama
cha watu wenye ulemavu mkoani Dodoma kimeitaka jamii kuhakikisha inawapekeleka
shule watoto wanaozaliwa na ulemavu wa aina yeyote ili kupatiwa haki yao ya
msingi .
Hayo yamebainishwa
leo na katibu wa chama cha watu wenye ulemavu mkoani Dodoma bwana Kalebi
Muhawi, wakati akizungumza na Dodoma FM habari juu ya tathmini ya kupewa nafasi
watu wenye ulemavu.
Amesema kuwa jamii
inapaswa kuondokana na imani za kuamini kuwa watu hao hawana uwezo wa kufanya
chochote katika jamii bali wajenge desturi ya kuwapeleka kupatiwa elimu kwani
ndio msaada wao mkubwa utakaowasaidia kupata uelewa wa namna ya kupambana na
maisha ya baadae.
Katika hatua
nyingine bw Mhawi amewataka waajiri wa taasisi za umma na binafsi kuondoa
unyanyapaa wa kuhisi kuwa kuajiri mtu mwenye ulemavu ni kuongeza mzigo kazini
bali pia watoe ajira kwa watu wenye ulemavu kwani wana uwezo wa kufanya kazi
kama wafanyakazi wengine.
Aidha ameiomba
serikali kuendelea kuboresha mazingira kwa watu wenye ulemavu kwa kuwatengezea
miundo mbinu rafiki kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na afya ili
kuwasaidia watu hao kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za
kimaendeleo.
Na Alfred
Bulahya Dodoma
FM
Comments
Post a Comment