
Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania TCRA imewataka
wanafunzi walioko chini ya umri wa miaka 18 kutojihusisha na suala la matumizi
ya mitandao wakiwa shuleni na badala yake kutumia muda huo kujifunza zaidi ili
kuwa watumiaji wazuri wa baadae.
Hayo
yamesema na naibu mkurugenzi wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka mamlaka
ya mawasiliano Tanzania TCRA Bw. Thadayo Ringo wakati akizungumza na wanafunzi
wa shule ya sekondari ya wasichana ya Msalato mjini Dodoma katika maadhimisho
ya siku ya haki na wajibu kwa watumiaji wa mitandao ambayo huadhimishwa kila
mwaka ifikapo march 15.
Awali akitoa elimu kwa watumiaji wa
huduma za mawasiliano afisa masafa kutoka ofisi ya mamlaka ya mawasiliano mjini
Dodoma Boniphace Ngeela amewaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza taarifa mbalimbali zinazoweza
kuleta mkanganyiko katika jamii kwani ni
wajibu wa kila mtumiaji kuhakikisha anatumia vizuri simu yake ili kuondoa adha
kwa watumiaji wengine.
Mkuu wa shule ya sekondari Msalato
Mwalimu Line Chanafi amepongeza hatua zinazofanywa na mamlaka ya mawasiliano za kuhakikisha
watumiaji wanatumia huduma za mawasiliano kwa usahihi huku akitumia nafasi hiyo
kuwataka wanafunzi wote kusoma kwa bidii ili kufika katika kilele cha mafanikio
waliyoyakusudia.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA
FM
Comments
Post a Comment