Imeelezwa kuwa
kubadilishwa kwa utungaji wa Mtihani wa kuhitimu Darasa la saba kwa mwaka 2018 kutoka maswali ya kuchangua pekee mpaka
mwaswali ya kuchagua na kujieleza kutawasaidia wanafunzi kujijengea uwezo wa
ufahamu.
Akiongea na Dodoma
Fm Afisa Elimu Msingi anaesimamia Taaluma katika Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma Mw. Mlavi Ramadhan amesema lengo la Baraza la Mitihani ni kutaka kupima
uelewa wa wanafunzi katika masomo wanayofundishwa darasani na kwamba mfumo uliopo utakuwa ni kipimo
tosha kwa mwanafunzi.
Mw. Ramadhan
amesema mara baada ya kupokea maelekezo hayo kutoka baraza waliwasiliana na
walimu wakuu na kuagiza kwa kila mazoezi ya mitihani yatakayotolewa kwa
wanafunzi yatungwe kwa kutumia mfumo
mpya uliotangazwa na baraza la Mitihani.
Sambamba na hayo
amewataka walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kufanya kazi kwa bidii
pamoja na kubadilisha mifumo yao ya ufundishaji na kufundisha kulingana na
muundo wa mitihani ya sasa itakavyotungwa.
March
20 mwaka huu baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) kupitia katibu mtendaji wa
Baraza hilo Dk Charles Msonde alisema Wanafunzi wa darasa la saba ambao watafanya mtihani mwaka huu
watakutana na mabadiliko ya mfumo wa utungaji wa mtihani wa kuhitimu
elimu ya msingi .
Na
Phina Nimrod Dodoma fm
Comments
Post a Comment