Wito
umetolewa kwa walimu nchini kuhakikisha wanajikita katika kutoa mafunzo yenye
uhalisia kwa wanafunzi yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zao za kimaisha .
Wito huo umetolewa Jana
na afisa elimu kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia bw Fundikira
Ekerele wakati akizungumza katika warsha fupi iliyoandaliwa na shirika la YOUNG SCIENTIST TANZANIA (YST)
linalojishughulisha na utoaji wa elimu ya sayansi kwa walimu iliyowakutanisha
walimu mbalimbali kutoka mikoa ya Dodoma
,Singida na Morogoro.
Amesema kuwa sera
mpya ya elimu na mafunzo imeweka msisitizo kwa walimu kujikita katika
ufundishaji utakaomjengea uwezo mwanafunzi wa kukabiliana na changamoto za
kimaisha anapomaliza masomo yake ili kuepusha wimbi la vijana wasiokuwa na kazi
mitaani.
Kwa upande wake
msimamizi wa elimu kutoka wizara ya elimu ofisi ya rais tawala za mikoa na
serikali za mitaa TAMISEMI BW Ndabazi Stephano amesema kuwa ili kufikia uchumi
wa kati ifikapo 2020 walimu na wadau wote wanatakiwa kuunga mkono juhudi
zinazofanyika katika kuboresha sekta ya elimu
nchini.
Meneja wa taasisi
ya Karimjee (JIANJEE FOUNDAION) bi Devota Rubama ambao ndio wafadhili wakuu wa
Shirika la YOUNG SCIENTIST TANZANIA (YST
amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
taasisi hiyo huku akitaja sababu zilizowasukuma kutoa ufadhili kwa shirika
hilo.
Taasisi YOUNG SCIENTIST TANZANIA (YST)
ilianzishwa mwaka 2011 kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wa shule za sekondari
kupata elimu ya sayansi na teknolojia inayotakiwa ili kupata wanasayansi mahili
watakaoweza kuja na masuluhisho mbalimbali ya matatizo yanayolikabili taifa la
tanzania.
NA
ALFRED BULAHYA DODOMA FM
Comments
Post a Comment