Walimu wanafaunzi wanaotarajia kujitolea
kufundisha katika shule mbalimbali katika kipindi chao cha likizo wametakiwa
kuonesha uwezo wao wa kufundisha .
Hayo yameelezwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mh. SELEMANI JAFFO wakati akizindua
Program ya walimu wanafunzi wanaokwenda kujitotea kufundisha katika shule
mbalimbali hapa nchini.
Jaffo ameahidi
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu hao na kwamba Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya utaratibu wa
kuwatengenezea vyeti vya shukrani ili
kuweka motisha kwa walimu wengine kujitolea.
Waziri Jaffo pia
amewataka walimu hao kutokukata tamaa katika mazingira yao ya kazi kutokana na
changamoto mbalimbali zinazozikabili shule mbalimbali ikiwemo uhaba wa vitendea
kazi pamoja na upungufu wa walimu wa sayansi.
Nae Mstahiki Meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
Devis Mwamfupe amewapongeza walimu hao kwa kitendo cha kijasiri
walichokionyesha.
Awali akimkaribisha
Mgeni Rasmi Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma DK. OMBENI MSUYA amesema
kuwa uamuzi wa kampeni ya
wanafunzi wanaosomea ualimu kujitolea ulikuja baada ya kuona upungufu mkubwa wa walimu katika shule
nyingi za serikali.
NaPhina
Nimrod Dodoma fm
Comments
Post a Comment