Kutokana na mkoa wa
Dodoma kuwa na joto kali,mvua kidogo imepelekea kushindwa kustawi kwa zao la pamba na wakulima kutakiwa kupanda
mazao ya mizizi kwani yanastahimili ukame likiwemo zao la mihogo.
Ushauri huo umetolewa na Afisa kilimo mkoa wa dodoma Benard
Abraham wakati akizungumza na Dodoma FM ambapo
amebainisha kuwa wakulima wanapaswa kupanda mihogo kulingana na hali ya mvua.
Amesema kukosekana kwa udongo wenye rutuba inayoendana na zao la
pamba,unyevunyevu wa kutosha na hali ya hewa nzuri imekuwa ni vigumu wakulima
kuotesha zao la pamba kwani linahitaji mvua zakutosha.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa siyo zao la pamba tu bali
kuna mazao mengi ambayo mikoa mingine yanapatikana lakini Dodoma hayasitawi.
Mazao ambayo yanastawi kwa Dodoma kutokana na hali yake kuwa ya
joto na mvua kidogo ni Mtama,Alizeti,Uwele,Zabibu pamoja na Ufuta
NA,MINDI JOSEPH DODOMA
FM
Comments
Post a Comment