Wakazi wa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wameishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wake.
Wakizungumza na Dodoma
FM Redio kupitia dawati la habari kwa
nyakati tofauti wakazi wa eneo hilo la Bahi wameipongeza serikali kwa
kuwatatulia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa mda mrefu ya huduma za afya na
miumndombinu ya barabara.
Nae diwani wa kata
hiyo bwana Augustino Ndonu akizungumza na Dodoma FM amesema mipango aliyokuwa
nayo kwa wananchi ilikuwa ni kuwasaidia kupata huduma bora za kijamii ikiwemo Bank,
Afya na barabara na kwa sehemu kubwa tayari yametekelezeka.
Mbali na hayo diwani
huyo amewataka wananchi na wanasiasa kuondoa tofauti zilizopo badala yake
washikamane kwa pamoja kuwaletea wananchi maendeleo.
Na
Victor Makwawa Dodoma FM
Comments
Post a Comment