
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto UMMY MWALIM amewataka
viongozi wa serikali za vijiji vyote Tanzania kuwaandikisha waganga wa kienyeji
waliopo katika maeneo yao kushirikiana kuwapata watu wenye ungojwa wa TB
waliopo maeneo mbalimbali ili kuwapatia matibabu bora zaidi.
Akizungumza na waandishi wa
habari mjini DODOMA Kuelekea maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ambayo
huadhimishwa kila ifikapo march 24, Waziri Ummy amesema Kutokana na ugonjwa wa
kifua kikuu kuwa tatizo kubwa hapa nchini wamekusudia kushirikiana na waganga
wa kienyeji ili wasaidie katika
kuwabaini wagonjwa wa kifua na kupewa matibabu stahiki.
Waziri UMMY amesema wanahitaji
kuongeza nguvu ili kukabiliana na
ugonjwa huo kutokana na ukubwa wa tatizo ambapo amethibitisha wagonjwa laki
moja na elfu sitini wamebainika huku asilimia aroboini pekee wamefanikiwa
kuwapatia matibabu.
Kwa upande wake Meneja mpango
wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma BEATRICE MUTAYOBA ameongeza kuwa
wamejipanga kutoa elimu ya kutosha hasa vijijni kutokana na ujenzi duni wa
nyumba zisizo na madirisha ya kupitisha hewa za kutosha na kutoa mafunzo kwa
waganga wa kienyeji,ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia
vitendea kazi kwa ajili ya kutoa rufaa.
Nae Mkurungezi wa kinga DR LEONARD
SUBI amebainisha waganga wa tiba asilia wanasajiliwa kisheria na serikali inaendelea kuhamasisha kushirikiana
na waganga wa tiba asilia.
Takwimu
za mwaka 2017 zinaonyesha kuwa mikoa 26 asilimia kubwa ya wagonjwa wa kifua
kikuu wanatoka mkoa wa Dar es salaam 20%,
Mwanza 6%, mbeya ,arusha,dodoma na morogoro 5% ikifuata na
Geita,Tanga,manyara,shinyanga na kilimanjaro 4%
huku katavi,ugunja na rukwa
zikiwa ni asilimia moja.
Waandishi Mindi Joseph na Hadija Halfani DODOMA FM
Comments
Post a Comment