Imeelezwa kuwa kuna umuhimu wa
kuwa na walimu maalumu waliopata mafunzo kwa ajili ya kufundisha darasa la
kwanza mpaka la tatu ili kujenga msingi mzuri kwa wanafunzi.
Hayo yamekuja
kufuatia ripoti ya mwaka 2017 ya upimaji wa kujifunza ya uwezo Tanzania,utafiti
uliolenga wanafunzi wa miaka 9 hadi 13
kuona iwapo wanaweza kufanya majaribio ya darasa la pili.
Dodoma fm
imezungumza na Dr Ombeni Msuya ambae ni
mdau wa elimu pamoja na Davis Makundi kutoka Shirika la Marafiki wa Elimu
Dodoma ambapo wamesema kuwepo kwa walimu walioandaliwa na kupewa jukumu la
kufundisha madarasa ya awali pekee kunaweza kusaidia kuwa na msingi imara kwa
wanafunzi.
Aidha wamewasihi
wazazi na jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao
shuleni ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kutatua changamoto zilizopo katika
shule nyingi.
Wameomba serikali kupitia
wizara ya elimu sayansi na teknolojia kupitia tafiti mbalimbali zinazofanywa
kuhusu elimu na kuona namna ya kutafuta suluhu juu ya matokeo ya tafiti
hizo.
Tafiti zilizofanywa
na uwezo Tanzania kupitia ripoti iitwayo je ,watoto wetu wanajifunza?imeonesha
kutokuwa na usawa kwenye mfumo wa elimu ambapo baadhi ya wilaya zimeonekana
kutokufanya vizuri katika majaribio hayo.
Mariam
Matundu
Dodoma Fm
Comments
Post a Comment