Viongozi
wa dini kwa kushirikiana na Taasisi ya Hope Delivary Foundation wanatarajia kufanya maombi maalum yenye lengo
la kuwaombea watu wenye Ualbino mjini Dodoma.
Akiongea na Dodoma
FM Mkurugenzi wa Taasisi ya Hope Delivary Foundation Bw. Michael Salali
amesema lengo la kufanya maombi hayo ni kuwaweka watanzania pamoja wakiamini yanaweza yakasaidia kumaliza ukatili unaofanywa kwa watu wenye ualbino na kupata nafasi ya kuishi kwa amani kama watanzania wengine.
Bwana Michael
amesema rekodi zinaonesha vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino hutokea miaka miwili kabla ya uchaguzi hivyo wameona ni vyema kuwashirikisha viongozi wa dini kutokana na nguvu kubwa waliyo nayo ya kukemea vitendo viovu.
Nae Mchungaji Erick
Mponzi wa Kanisa la Moravian Dodoma ambalo
mamombi yatafanyika hapo amesema matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino
yamekuwa yakiendelea kutokea kutokana na
uvivu wa watu kutaka kupata mali kwa njia za kishirikina na kwamba ni vizuri
kuyakemea na watu kufahamu njia pekee ni
kufanya kazi na kumuomba Mungu.
Maombi maalumu kwa
ajili ya kuwaombea watu wenye ualbino yatafanyika mwishoni mwa wiki hii March 25 na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Siasa.
Na
Phina Nimrod
Dodoma FM
Comments
Post a Comment