
Makundi
ya vijana wanaofanya uhalifu yameibuka katika kata ya kizota Manispaa ya Dodoma
na kupelekea hali ya usalama kutokuwa nzuri.
Akizungumza na
Dodoma FM Kupitia Taswira ya habari Afisa mtendaji wa kata ya Kizota Bi LOYCE JOEL amesema yapo makundi ya vijana kutoka katika mitaa
tofauti iliyoko katika kata hiyo kwa kushirikiana na makundi mengine kutoka
maeneo jirani na Kizota hutekeleza uhalifu huo hasa nyakati za usiku kwa
kuvunja milango na kupora baadhi ya mali za wananchi pindi wanapokuwa wamelala.
Bi LOYCE amesema
kutokana na doria inayofanywa na polisi jamii kwa kushirikiana na polisi kata
imebainika kuwa makundi hayo yanaundwa na vijana kutoka mitaa ya Mbuyuni na Sokoine
huku kundi shiriki kutoka jirani likiwa linatokea Chinangari West.
Amesema makundi
hayo ya uhalifu yanashirikisha vijana wadogo kwani wengi wao wako kati ya umri wa miaka 16-18 huku akikemea kitendo cha
kutolewa kwa dhamana pindi wanapokamatwa na kufikishwa polisi jambo ambalo
amesema linapunguza adhabu kwani ilitakiwa wawe wanakaa angalau miezi sita ili
kujifunza na kujirudi kimakosa.
Afisa mtendaji huyo
ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwakanya vijana hao kwani bado wanahitaji
malezi kutoka kwao kulingana na umri wao kuwa mdogo kwani kwa kutofanya hivyo
sheria itachukua mkondo wake na kuwatia hatiani.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA
FM
Comments
Post a Comment