Mwenyekiti wa umoja
wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa amewataka vijana mkoani Dodoma kutumia
fursa ya serikali kuhamia Dodoma kwa kufanya kazi mbalimbali zitakazo wasaidia
kunufaika na uwepo wa serikali.
Bwana Heri James ametoa
kauli hiyo mapema leo alipokuwa akizungumza katika kikao maalumu
kilichowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.
Amesema kuwa wakati
wizara mbalimbali zinaendelea kuhamia
mkoani Dodoma hivyo vijana
wanapaswa kuanza kufikiri ni namna gani watatumia fursa hiyo kujipatia
manufaa.
Aidha amewataka
vijana wote kuwasaidia viongozi wao katika kutekeleza majukumu yao sambamba na
kutoa taarifa za viongozi wa serikali wanaokwamisha shughuli mbalimbali za
maendeleo nchini ili hatua ziweze kuchuliwa.
Kwa upande wake
mbunge wa vijana mjini Dodoma bi Mariamu Depotile amesema kuwa amekwisha
kupeleka maombi serikalini kutunga sheria ya makao makuu itakayowasaidia vijana
kutambulika kisheria ili kurahisisha upatkanaji wa fursa zitazojitokeza mkoani
hapa.
NA
Alfred Bulahya DODOMA
FM
Comments
Post a Comment