Wazazi na walezi wameshauriwa kuwakemea watoto wao wa kike juu ya kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo ili kuepukana na mimba za utotoni.
Akizungumza na
Dodoma fm Afisa elimu wa sekondari
manispaa ya Dodoma Bwana ABDALLAH MEMBE amesema wazazi na walezi wana jukumu la kuwalea kimaadili watoto wao ikiwa ni pamoja kuwakataza kujihusisha
na mapenzi wawapo masomoni.
Kauli hiyo imekuja
wakati Afisa elimu akizungumza juu ya
upimaji mimba shuleni pindi wanafunzi
wanapotoka likizo .
Afisa huyo wa elimu
amesema wapo baadhi ya wazazi ambao huwashauri watoto wao wa kike kutumia uzazi
wa mpango jambo ambalo sio zuri kwani
ukiachilia kupata mimba pia mtoto anaweza kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI.
Aidha bwana Membe
amesema swala la upimaji mimba shuleni linamsaidia mwanafunzi kujilinda na
vishawishi vya kimapenzi awapo masomoni kwani huzitambua adhabu zake mapema ikiwemo
kufukuzwa shule iwapo atagundulika kuwa na ujauzito.
Katika hatua
nyingine Bwana Membe ameunga mkono hoja
iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Afya UMMY MWALIMU juu ya kuwapima
ugonjwa wa kifua kikuu wanafunzi wanaoanza masomo katika shule za kulala, kwa
kusema ni mipango mizuri ya serikali ya udhibiti dhidi ya magonjwa ya kuambukiza.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment