Ukosefu wa huduma ya choo
katika eneo la kituo cha mabasi cha halmashauri ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
kuna hatarisha usalama wa afya za wananchi wanaofika katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Mtaa
wa Mnyakongo shuleni katika Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma Bw. Moses Patson
ameiambia Dodoma fm kuwa kufutia kuanzishwa kwa huduma ya stand katika Wilaya
ya Kongwa bila huduma ya vyoo ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia kutokea
kwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Amesema Kutokana na
wingi wa watu pamoja na ukubwa wa eneo la stendi ni vema uongozi wa Halmshauri
ya Wilaya ya Kongwa ukaanza ujenzi wa matundu ya vyoo katika eneo hilo ili
kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Kongwa Mhandisi Ngusa Izengo
amesema katika stendi hiyo kuna choo
kilicho jengwa na kubinafisishwa kwa ajili ya usimamizi na kutokana na wingi wa
watu uliopo kwa sasa Halmashauri ya Wilaya hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa
choo kikubwa kitakachotosheleza mahitaji ya wananchi katika eneo hilo.
Mhandisi Igezo
amewasihi wananchi kujenga mazoea ya kuchangia kiasi cha fedha kilichoelekezwa
na uongozi wa halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na kuepuka kujisaidia hovyo
katika maeneo yasiyokuwa rasmi ili kuepusha vimelea vya magonjwa ya kuambukiza
ikiwemo kipindupindu.
Na
Pius Jayunga
DodomaM
Comments
Post a Comment