Imeelezwa kuwa ukosefu wa fedha
za miradi ya maendeleo katika sekta ya mawasiliano kimekuwa chanzo
kinachokwamisha kukamilika kwa shughuli za maendeleo katika jamii.
Hayo yamebainishwa na
katibu mkuu wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano Bi Maria Sasabo wakati
akifungua mkutano wa baraza la wafanya kazi wa sekta ya mawasiliano mjini
Dodoma.
Bi Sasabo amesema
kuwa kukosekana kwa fedha za miradi ya maendeleo katika sekta hiyo kumekuwa
kukichangia kwa kiasi kikubwa kuchelewa kukamilika kwa wakati baadhi ya miradi
iliyopangwa hivyo juhudi za makusudi zinapaswa kufanyika ili kumaliza tatizo
hilo.
Aidha Katibu huyo amewataka
viongozi wa idara na vitengo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ,kwa kutoa
huduma bora kwa jamii kulingana na vigezo vilivyowekwa na wizara ili kuepusha
kuchukuliwa hatua kali kwa wafanyakazi wanaoshidwa kutekeleza majukumu yao.
kwa upande wake
mwanasheria kutoka katika sekta ya mawasiliano mjini Dodoma Bi Yunisi Masiguti amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na taarifa za uongo
zinazotumwa mitandaoni kwa nia ya kudhuru au kudanganya ili kuepusha matukio
mbalimbali ya uvunjifu wa amani yanayokuwa yakisababishwa na taarifa hizo.
Na Alfred Bulaya DODOMA FM
Comments
Post a Comment