
Imeelezwa kuwa hivi karibuni
serikali itaviamisha vituo vya magari makubwa na madogo na kuvipeleka nje ya
mji, kwa lengo la kupisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi ikiwa ni azma ya
serikali ya awamu ya tano.
Hayo yamesemwa na
afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA Mkoa
wa Dodoma Bwana Konrad Shio wakati akizungumza
na Dodoma FM Habari ambapo amesema kuwa kwa kuanza hivi karibuni vituo vyote
vya magari makubwa na madogo vitafungwa kwa ajili ya kumpisha mkandarasi ili
kuanza kwa hatua za awali za ujenzi huo.
Amesema zoezi ilo
awali lilipangwa kuanza kutekelezwa mnamo mwaka jana ila
halikufanyika,nakuwataka madereva kufuata sheria pindi muda utakapofika.
Bwana shio amesema
SUMATRA imejipanga kuweka utaratibu
utakaowaongoza wageni pindi watakapofika ndani ya mkoa ili kuendana sawa na
utaratibu wa mikoa mingine.
Aidha afisa huyo
ametoa wito kwa madereva kufuata sheria walizopangiwa kwani kutofanya hivyo ni
kosa na atakayebainika
atachukuliwa hatua za kisheria.
Na Rwekaza Katebalilwe DODOMA FM
Comments
Post a Comment