
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma
zimetajwa kuharibu miundombinu ya barabara katika kata ya Ilazo manispaa ya
Dodoma na kupelekea changamoto kubwa kwa wakazi waishio maeneo hayo.
Akizungumza na kituo hiki mwenyekiti wa kata hiyo Bi Baby Mavuga
amesema mvua hiyo imeleta athari katika kata hiyo kufuatia barabara zote katika
kata hiyo kuharibika .
Bi Mavuga amesema wakazi wengi waishio katika kata ya Ilazo wana
usafiri ikiwemo magari pamoja na pikipiki hivyo wanalazimika kuacha usafiri wao
na badala yake kutembea kwa miguu.
Hata hivyo Dodoma FM imemtafuta diwani wa kata hiyo Bwana Kavuli Gombo
ambapo amesema tatizo kubwa maji yote yanayotoka maeneo ya mjini yanaelekea
katika kata hiyo hivyo kusababisha adha hususani kwenye barabara zilizo na
changarawe.
Diwani huyo amesema tayari TARURA wanajua ubovu wa miundombinu hiyo
hivyo wanasubiri kumalizika msimu wa mvua ndipo waanze kuboresha miundombinu ya
barabara.
Na Beny Bert
Dodoma Fm
Comments
Post a Comment