Mvua
zinazoendelea kunyesha na kutokuwepo kwa miundombinu muhImu katika eneo la Nanenane
mjini Dodoma zimesababisha zoezi la kuhamisha standi ya mabasi kama ilivyokusudiwa.
Akizungumza na Dodoma
FM Radio Afisa mfawidhi wa mamlaka ya
udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra mkoa wa Dodoma bwana Konradi
Shio amesema awali zoezi hilo lililokuwa lifanyike wiki iliyopita halikufanyika
kwa kutokuwepo na miundombinu rafiki katika eneo hilo huku akiitaja miundombinu
hiyo kuwa ni eneo la kukaa abiria wakati wa mvua, umeme, vyoo pamoja na njia za
kupita mabasi.
Bwana Shio amesema Sumatra mkoa wa Dodoma kwa
kushirikiana na wadau wengine likiwemo jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani wanaendelea na utaratibu wa kutengeneza mazingira rafiki kwani
wanaandaa kituo kidogo cha magari maalumu yatakayokuwa yanasafirisha abiria
kuelekea katika standi ya muda ya mabasi makubwa ili kuwaepushia gharama
kubwa abiria kama kukodi pikipiki bajaji au taksii ili kuelekea
kituoni hapo.
Bwana Shio mesema
kwa mujibu wa muda wa wiki moja uliyoombwa na wamiliki wa mabasi kuendelea
kuwepo katika standi inayotumika kwa sasa umeisha hivyo zoezi la kuhamisha
standi hiyo linatarajia kufanyika kunako wiki hii kwa mujibu wa maelekezo.
Na
RWEIKIZA
KATEBALIRWE DODOMA
FM
Comments
Post a Comment