
Katika kipindi cha mwaka 2016
hadi 2017 Tanzania imepanda hadi kufikia nafasi ya 13 katika mapambano dhidi ya
vitendo vya rushwa kwa mjibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Transparency
International mapema mwezi wa pili mwaka huu.
Msemaji mkuu wa
serikali Dr. Hassan Abbas ameyasema
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mapambano hayo ya
kupinga vitendo vya ufisadi nchini imekuwa chachu ya viongozi kuwajibika katika
nafasi zao na utoaji wa huduma stahiki kwa wananchi bila upendeleo.
Amesema awali
Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 216 na baada ya kupanda kwa nafasi 13
imefikia nafasi ya 203 na kutokana na mapambano hayo ya ufisadi fedha za umma
zimekuwa zikitumika kwa matumizi stahiki na kwa manufaa ya wengi.
Amesema kwa mjibu
wa ripoti hiyo Tanzania inashika nafasi ya pili katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki na matarajio ya Serikali ni kupanda kwa nafasi ya juu katika
mapambano dhidi ya rushwa kwa kushirikiana na jamii katika kubainisha uwepo wa
vitendo hivyo katika nyanja mbambali.
Na
Pius Jayunga
Dodoma FM
Comments
Post a Comment