TANZANIA YAADHIMISHA MAADHIMISHO YA HALI YA HEWA NA KUITAKA JAMII KUWA NA IMANI NA UTABIRI UNAOTOLEWA
.jpg)
Imeelezwa
kuwa ili kuondokana na majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko na ukame mamlaka
husika na jamii zinapaswa kutunza mazingira ipasavyo ikiwa ni pamoja na
miundombinu iliyopo nchini.
Waziri wa ujenzi
uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbarawa ameyasema hayo leo mjini Dodoma
katika kusherehekea siku ya mamlaka ya hali ya hewa duniani ambapo amesema
jamii inapaswa kutunza mazingira ili kupunguza changamoto za mafuriko na ukame.
Amesema jamii na mamlaka
husika zinatakiwa kuchukua tahadhari pindi zinapopata taarifa za mamlaka ya
hali ya hewa kwa kuandaa miundombinu rafiki itakayoweza kuzuia maafa kutokea.
Katika kufanikisha
hayo Waziri Mbarawa amesema serikali
itaendelea kuiwezesha mamlaka ya hali ya hewa kwa kila hali ili iendelee kutoa
taarifa za uhakika zitakazosaidia kukuza uchumi katika nchi.
Nae mkurugenzi wa
mamlaka ya hali ya hewa nchini Agnes Kijazi amesema mamlaka ina vifaa
vinavyowezesha kutoa taarifa za usahihi na kwamba kwa mujibu wa makubaliano ya
kimataifa utabiri ukiwa na usahihi wa 70% unaweza kutumika kwa maendeleo.
Mamlaka ya hali ya
hewa imeazimisha miaka 68 tangu kuanzishwa duniani ambapo ilianzishwa march 23
mwaka 1950 na kwa Tanzania mamlaka hii
ilianzishwa mwaka 1999 ,na imebebwa na kaulimbiu JIWEKE TAYARI NA ZINGATIA
TAARIFA ZA HALI YA HEWA.
Mariam
Matundu
Dodoma FM
Comments
Post a Comment