
Siku moja baada ya waziri wa
fedha na mipango Dr. Philip Mpango kutoa takwimu za makisio ya idadi ya watu
Nchini Serikali imeshauriwa kuwekeza katika sekta ya kilimo na viwanda ili
kuendana na idadi ya ongezeko la watu.
Mchambuzi wa masuala
ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Iringa Pr. Enock Wiketye ameiambia Dodoma fm
kuwa ongezeko la watu Nchini linapaswa kwenda sambamba na kukua kwa uchumi
Nchini ili kukidhi mahitaji.
Amesema uzalishaji
mali unapaswa kuimarishwa katika sekta ya kilimo na viwanda kwa kuwawezesha
wakulima kuendesha kilimo chenye tija tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo 70% ya
wakulima wanaendesha kilimo cha jembe la mikono, 20% wakiendesha kilimo cha
jembe la kukokota na ng’ombe huku 10% pekee wakiendesha kilimo cha kukokota na
trekta.
Kwa mjibu wa taarifa ya makisio ya idadi ya watu iliyotolewa
na waziri wa fedha na mipango Dr. Phillip Mpango inaonesha viwango vya uzazi na
vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya watu nchini ikiwa ni milioni 54.2 ambapo Tanzania Bara
ni watu milioni 52.6 na
Tanzania visiwani watu milioni 1.6 kwa
mwaka 2018.
Kutokana na makisio
hayo Prof. Wiketye amesema idadi ya watu waliopo Nchini sehemu kubwa ikiwa ni
kundi la vijana ambao wanahitaji kupata ajira ili kujipatia kipato kupitia
sekta mbalimbali hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mikakati thabiti ya kukuza
uchumi kupitia sekta ya kilimo na viwanda.
Tanzania inakuwa
nchi ya 6 kwa idadi kubwa ya watu Barani Afrika baada ya Nigeria, Ethiopia, DRC pamoja na Misri
kuwa na idadi kubwa ya watu.
Na Pius Jayunga Dodoma Fm
Comments
Post a Comment