
Tanzania imefanya vizuri katika utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 hali iliyopelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa homa ya mapafu kwa watoto.
Naibu
waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta Faustine Ndugulile
amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na Dodoma FM Redio juu ya tathmini ya
hali ya homa ya mapafu kwa watoto.
Dokta
Faustine amesema Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la afrika kufanya vizuri
katika utoaji wa chanjo kwa watoto.
Amesema
watoa huduma katika sekta ya afya wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika
kupambana na homa ya mapafu na kuwataka waendelee kuwahimiza wazazi kuwapeleka
watoto kliniki ili kupata chanjo.
Wazazi
wametakiwa kutambua umuhimu wa kuwapeleka watoto wao klinik ili kupata chanjo
mbalimbali ikiwemo ya kuzuia homa ya mapafu kwa watoto (nimonia) kwani ugonjwa
huu umekuwa ukiwakumba zaidi watoto walio na umri chini ya miaka 5.
Mariam Matundu Dodoma
FM
Comments
Post a Comment