
Wananchi wakumbushwa kusafisha
mazingira na kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka ugonjwa wa ngiri maji
unaosababishwa na mdudu aina ya mbu.
Hayo yameelezwa na
daktari kutoka kituo cha afya cha Makole manispaa ya
Dodoma DR.GRAYSON JULIUS NDALAMA wakati akizungumza na Dodoma FM
ambapo amesema ugonjwa wa Ngiri maji ni kama malaria na kuwasihi
wananchi wazingatie usafi katika mazingira yanayo wazunguka na kutumia vyandarua kwa umakini.
Hata hivyo Dokta
GRAYSON amesema awali ugonjwa huo ulikuwa unawapata kwa kiasi kikubwa watu wa
pwani lakini sasa hivi imekuwa tofauti kwani
ugonjwa huo unaweza kumpata mtu kutoka sehemu yoyte.
Dokta GRAYSON
amesema ugonjwa huo ni miongoni mwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na
kuongeza kuwa ugonjwa huo unawakuta watu wenye maisha ya hali ya chini huku
akisema hauchagui jinsia.
Pamoja na hayo
amesema wana kampeni ya kugawa dawa kwa ajili ya kinga tiba ya ugonjwa huo
ambayo unatakiwa kumeza kila baada ya miezi mitatu.
Kulingana na takwimu za mwaka
2016 serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilisema watu milioni 47 wapo katika
hatari ya kupata magonjwa ya Matende, Ngiri Maji na Kichocho nchini Tanzania
huku wengine milioni 6 wakiwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa usubi.
Na
Benard Filbert Dodoma FM
Comments
Post a Comment