
Mamlaka ya udhibiti
usafirishaji wa nchi kavu na majini SUMATRA inatarajia kuanza kutoa leseni kwa
makampuni na vyama vya ushirika mkoani Dodoma ili kuboresha huduma za usafiri
hasa wa daladala.
Maazimio hayo
yamekuja kufuatia kikao cha wamiliki wa daladala na SUMATRA mkoani Dodoma ambapo
imeleezwa kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kuboresha usafiri huo ili kuendana
na mabadiliko ya kuijenga makao makuu.
Akizungumza katika
kikao hicho meneja leseni SUMATRA Leo
John Ngowi amesema kuwa mpaka kufikia April Mosi mamlaka inatarajia kuanza
kutoa leseni katika makampuni ili kutoa huduma ya usafiri sambamba na kufuta
vituo vya daladala vilivyopo mjini na badala yake daladala zifanye mzunguko.
Aidha amesema kuwa
kutokana na mji wa Dodoma kuwa na ongezeko la watu SUMATRA imeamua kuwa na magari
aina ya costa zitakazofanya kazi ya kusafirisha abiria katikati ya mji na
daladala zitapelekwa pembezoni mwa mji.
Baadhi ya wamiliki
wa daladala wamepata wasiwasi juu ya umbali kutoka kituo kimoja hadi kingine
lakini pia biashara ya mzunguko bila kukaa katika kituo kimoja huenda ikaharibu
biashara yao kwa kupata hasara.
Akijibu hoja hizo
afisa mfawidhi sumatra amesema kuwa kwasasa hakuna haja ya kujadili juu ya hilo
bali ni kuanza kuutumia mfumo huo na iwapo kasoro zitajitokeza watajua namna ya
kukabiliana nazo.
Mariam
Matundu
Dodoma FM
Comments
Post a Comment