Skip to main content

SITA MTIBWA SUGAR WAITWA NGORONGORO HEROES KUIVAA KONGO

                       Image result for Ngorongoro Heroes 

NYOTA sita wanaotumikia kikosi cha Mtibwa Sugar wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana (Ngorongoro Heroes) kwa ajili kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2019 chini ya umri wa miaka 20.

  Nyota walioitwa ni kipa wa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar Abuutwalib Msheli, Kibwana Ally Shomary (beki wa pembeni), Dickson Mwakasisili Job (beki ya kati) na Riphat Khamis Msuya (mshambuliaji).

  Wachezaji wengine wawili ni Nickson Clement Kibabage (beki) anayetumikia kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6 na Muhsin Makame Malima (kiungo mshambuliaji) anatumikia kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6.

 

Mtibwa Sugar ime endeleza utamaduni wake wa kukuza vipaji na kikosi kilichoitwa cha Ngorongoro Heroes  ni timu iliyo ongoza kwa kutoa wachezaji wengi katika kikosi cha Ngorongoro Heroes jumla ya wachezaji 6 wameitwa katika kikosi hicho.

 
Ngorogoro Heroes chini ya Kim Poulsen na Oscar Milambo wanatafuta nafasi ya kufuzu katika michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Nigeria mwakani.

 
Ngororo Heroes wana kibarua Machi 30 dhidi ya DR Congo jijini Dar es laam na baadae Ngorongoro Heroes watasafiri hadi Kishasa Congo Aprili 22 kwa ajili ya mchezo wa marudio

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...