
Serikali
imekiri kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue baada ya kukamilika kwa vipimo
vilivyofanywa katika maabara ya Taifa kufuatia kupokelewa sampuli kumi na tatu
za damu kutoka Hospital ya International School of Tanganyika (IST) iliyopo
Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu ameyasema hayo March
21,2018 wakati akizugumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa kati ya
sampuli kumi na tatu za damu zilizofanyiwa vipimo sampuli kumi na moja
zilionesha kuwa na ugonjwa wa Dengue.
Kufuatia kuwepo kwa
ugonjwa huo Nchini Serikali kupitia wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia
wazee na watoto imetoa taarifa kwa waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya Tanzania
Bara ili kuzitambua dalili za ugonjwa huo na kwamba ugonjwa wa dengue uliwahi
kuripotiwa hapa Nchini mwaka 2010, 2013 na 2014.
Waziri Ummy amesema
homa ya Dengue inasababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aina ya Aedes weusi
walio na madoa meupe yanayo ng’aa huku dalili za ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na
homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na
uchovu, na dalili hizo huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi siku kumi na nne
tangu mtu alipoambukizwa.
Aidha Waziri Ummy
amesema kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo hakuna vikwazo vyovyote vilivyotolewa
kwa wasafiri wanaoingia na kutoka Nchini na kwamba shughuli za usafiri wa
kuingia na kutoka Nchini zinaendelea huku jitihada mbalimbali zikichukuliwa ili
kutokomeza ugonjwa huo.
Na
Pius Jayunga DODOMA FM
Comments
Post a Comment