Imeelezwa kuwa
uhaba wa madarasa shuleni wanafunzi kutofika shule kwa wakati kutohudhuria darasani
wakati wa vipindi na utoro, ni changamoto zinazosababisha ufaulu mdogo na hivyo
kushuka kitaaluma kwa mwanafunzi.
Hayo yamebainishwa na
mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Kizota iliyopo manispaa ya Dodoma Bi
Olimpia Mpunga wakati akizungumza na Dodoma
FM juu ya sababu za shule hiyo kushuka kitaaluma.
Mwl Olimpia amesema
upungufu wa vyumba ya madarasa unawafanya wanafunzi kusoma kwa awamu ili kupeana nafasi, jambo ambalo ni changamoto kubwa.
Mwalimu
Olimpia amebainisha kuwa sababu
zinazosababisha kuwepo kwa utoro kwa wanafunzi shuleni hapo ni pamoja na wanafunzi kuwa na makundi mitaani na wengine kuwa na visingizio vya kuwa na
matatizo .
Aidha amesema
tayari wanao mpango mkakati wa kudhibiti utoro huo kwa kushirikiana na shirika
la WWU ambao linashirikisha wazazi na walimu na kuwa kazi ya wazazi ni kujadili
mbinu za kutumia katika kudhibiti utoro na mbinu za kuleta maendeleo katika
taaluma.
Kwa upande wao
wanafunzi wamewaasa wanafunzi wenzao ambao wamekuwa na tabia ya utoro kwenye
vipindi na wengine kutohudhuria shuleni kuwa ni vyema wakajijengea mazoea ya
kwenda shule kwani wasipohudhuria
vipindi darasani hukosa uelewa wa baadhi ya masomo na hivyo kufeli katika
mitihani yao ya mwisho
Rweikiza
katebalirwe
Dodomafm
Comments
Post a Comment