Mkuu
wa mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge ameagiza kuchukuliwa hatua kali za
kisheria watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Dodoma wanaokwamisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Ametoa agizo
hilo katika kikao cha kamati ya ushauri
ya mkoa wa Dodoma kufuatia wilaya ya Mpwapwa kufanya vibaya katika ukusanyaji
wa mapato na kushika nafasi ya mwisho kati ya halmashauri zote za mkoa wa
Dodoma.
Amesema wilaya ya
Mpwapwa ni kongwe lakini anasikishwa na vitendo vya baadhi ya watendaji wasio
waaminifu na kupelekea mpwapwa kuwa na asilimia 24 za ukusanyaji wa mapato.
Aidha Mkuu wa mkoa
amewataka watendaji hao kubadilika ili kukuza hali ya ukusanyaji wa wa mapato
yanayokusanywa kwa ajili ya kuboresha miradi kama vile maji,huduma za afya
,elimu na miundombinu mbalimbali ya maendeleo.
Wakati huo huo RC
Mahenge amewahimiza watendaji kuanzia ngazi ya wakurugenzi,wakuu wa wilaya na
maafisa mipango miji kusimamia yote
waliyokubaliana ikiwemo vyanzo vipya vya
mapato na kusimamia vilivyopo na kuhakikisha
fedha inayopatikana inatumika katika malengo yaliyokusudiwa.
Pia mkuu wa mkoa amewazungumzia baadhi ya watumishi
wanaohamishwa vituo vya kazi kwa utendaji usioridhishwa kwamba hawastahili
kupangiwa vituo vingine vya kazi kutokana na kutokidhi matarajio katika vituo
vyao vya awali.
Na ANIPHA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment