Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kwenye
ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa na ya mwendo kasi, katika kipande cha kutoka
Mororgoro kuelekea mjini Dodoma .
Akiongea na Dodoma
FM Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith
Mahenge amesema kuwa zoezi hilo litafanyika mapema kesho machi 14 katika eneo
la kituo cha reli cha Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Amewataka wananchi
mjini hapa kujitokeza kwa wingi ili kumuunga mkono rais Magufuli kwani reli
hiyo itawasaidia wakazi wa Dodoma kupata
ajira, sanjari na kuongeza wawekezaji watakaotokana na urahisishaji wa
usafirishaji wa bidhaa utakaokuwa ukifanywa na Treni ya kisasa.
Aidha DK Mahenge amewatoa
hofu wananchi juu ya namna ya kufika katika eneo la Ihumwa akisema kuwa
kutakuwa na treni zitakazobeba wananchi kuwapeleka katika eneo husika huku
akitaja ratiba na muda wa treni hizo kuondoka itakuwa ni majira ya usiku.
Hata hivyo kituo
hiki kimezungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma ambapo wamesema kuwa mradi
huo utasaidia kurahisisha suala la usafiri kutumia muda mfupi ukilinganisha na
usafiri wa magari huku wengine wakimuomba Mh.Raisi kutumia fursa hii kutatua
changamoto mbalimbali zilizopo mkoani Dodoma .
Na Alfred Bulahya Dodoma FM
Comments
Post a Comment