RAIS MAGUFULI AZINDUA MAGARI 181 KATIKA BOHARI YA DAWA MSD YATAKAYOSAFIRISHA DAWA MIJINI NA VIJIJINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Magufuli amewataka viongozi wa dini kutumia madhabahu yao
kuhamasisha ujenzi wa viwanda ili kuepusha matumizi makubwa ya fedha za kununulia
dawa nje ya Nchi.
Rais Magufuli
ametoa kauli hiyo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu
ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali Nchini hafla iliyofanyika
leo katika eneo la keko Jijini Dar Es Salaam.
Rais magufuli
amesema zoezi la ununuaji wa dawa nje ya nchi linasababisha Nchi kupoteza fedha
zaidi ya Sh. Bilioni 500 kila mwaka, fedha ambazo zingebaki Nchini ili kuchangia
katika masuala mengine iwapo viwanda vya kuzalisha dawa Nchini vingekuwepo.
Aidha Mh. Rais
Magufuli amelipongeza shirika la Global Fund kwa jitihada zake katika kuendelea
kutoa huduma ya vifaa tiba kwa wananchi wa Tanzania na kwamba misaada hiyo
inachangia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Waziri
wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema kwa
sasa chanjo za watoto zinapatikana kwa kiwango kikubwa Nchini huku mkurugenzi
wa bohari ya dawa nchini (MSD) Laurian Bwanakunu akiweka wazi kuwa bajeti ya
dawa kwa mwaka 2017/18 imechangia kusambaza dawa zenye thamani ya sh. Bilioni
18 kila mwezi.
Bohari
kuu ya dawa (MSD) ina jumla ya kanda za maghala yapatayo kumi nchini kote
ambazo zinatumika kuhifadhia dawa.
Na Pius
Jayunga Dodoma
FM
Comments
Post a Comment