
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa 'Standard
Gauge' katika eneo la Ihumwa Mkoani Dodoma.
Katika hotuba yake
Rais Magufuli amesema ujenzi wa reli hiyo unatarajiwa kurahisisha usafirishaji
wa mizigo na abiria kwa wakati tofauti na ilivyo katika reli ya zamani ambayo
huchukua masaa zaidi ya 11 hadi 12 kwa kutumia reli iliyopo.
Aidha Rais Magufuli
amesema moja ya changamoto zinazolikabili Bara la Afrika ni pamoja na
kukosekana kwa miundombinu imara na ya uhakika kwa ajili ya usafirishaji na
kusababisha gharama za usafiri kuwa juu tofauti na mabara mengine Duniani.
Akizungumza katika
uzinduzi wa mradi huo Waziri mkuu Kasimu Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya
tano itaendelea kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa kuzingatia ilani ya
chama cha mapinduzi na kuwasihi wananchi kuwa wasimamizi wa karibu katika
miradi hiyo.
Awali akitoa
taarifa ya ujenzi wa mradi huo mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Tanzania TRC
Bw. Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli hiyo ni sehemu ya pili yenye
vipande vitano kutoka Dar es salaam hadi Morogoro kilometa 300, Morogoro,
Dodoma hadi Makutupora kilometa 422, Makutupora hadi Tabora kilometa 244,
Tabora hadi Isaka kilometa 134, na Isaka hadi Mwanza kilometa 441.
Mkataba wa ujenzi
wa sehemu ya pili ya reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Dodoma katika eneo la
Makutupora ulisainiwa mwaka 2017 kwa gharama ya dola milion. 1.923 sawa na
Trilioni 4.3 za kitanzania ikijumuisha kodi ya Serikali huku ujenzi huo
ukitarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 kuanzia februari 26 mwaka huu.
Na
Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment