
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa
TAMISEM kuwasimamisha kazi wakurugenzi
wa Halimashauri mbili kwa
kuongoza kuwa na hati chafu Nchini.
Rais Magufuli
amefikia uamuzi huo leo Ikulu Jijini Dare S Salaam baada ya kupokea
taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa
Assad ripoti iliyobaini mapungufu katika halmshauri hizo juu ya zoezi la
ukusanyaji wa mapato.
Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Bw.
Boniface Nyambe aliekuwa mkurugenzi wa Halamashauri ya Kigoma Ujiji, Bw.
Daud Mlahagwa aliekuwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Pangani ili kupisha
uchunguzi juu ya taarifa hiyo.
Aidha Rais Magufuli
ameikabidhi taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa na kuagiza kupitiwa kwa taarifa hiyo kipengele
kimoja baada ya kingine kupitia Baraza la Mawaziri, Ma Naibu mawaziri pamoja na
makatibu wakuu wote wa wizara.
Awali akikabidhi
taarifa hiyo kwa Mh. Rais mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)
Profesa Mussa Assad amesema kuwa deni la Taifa linafikia Sh. Trilioni 46
kutoka Sh. trilioni 41 la mwaka jana, na kwamba ni ongezeko la asilimia 12,
huku akishauri kufanyika ufuatiliaji katika baadhi ya taasisi zilizopewa ripoti
ya ukaguzi.
Kwa upande wake
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ameahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa na
wenyeviti wa kamati za Bunge ili kuhakikisha madhaifu yaliyojitokeza taarifa
hiyo hayajirudii tena katika kipindi kijacho.
Na Pius Jayunga
Dodoma FM
Comments
Post a Comment