
Katika mwendelezo wa mapambana
dhidi ya uharifu mkoani Dodoma jeshi la polisi limekamata matukio zaidi ya
manne na tayari baadhi ya watuhumiwa wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo.
Akizungumza na
wanahabari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma GILLESI MURUTO amesema
katika tukio la kwanza gari namba T 442 CVK aina ya fuso lililokuwa likiendeshwa
na dereva jina lake Bade Sanga (32)mkazi wa iringa limekamatwa likiwa
linawasafirisha wahamiaji haramu kutoka Rwanda kwenda Zambia akiwemo Wamotoni
Angelina (23)na Lilian Uwusa (26) wote wanawake raia wa kigeni.
Katika tukio
jingine gari namba T838 aina ya scania limekamatwa likiwa limebeba lobota nne
za mali ghafi za kutengeneza mabati likiwa linatoka jijini Dar -es-Salaam kuelekea
nchini Rwanda japo dereva wa gari hilo hajaonekana.
Aidha katika tukio
jingine kamanda MURUTO amesema jeshi hilo limekamata bima feki zilizokuwa
zinatolewa na Yusufu Ramadhani ambaye sio mkazi wa Dodoma na tayari bima hizo
zilikuwa zimetolewa kwa magari kumi na matano,pikipiki mbili, bajaji tano na
mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo.
Pamoja na hayo
polisi wanaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari makubwa huku magari madogo
zoezi likitaraji kuanza hii leo mpaka pale tarehe ya mwisho itakapotangazwa.
Na
Rwekiza .. Dodoma Fm
Comments
Post a Comment