Nyumba 62 na vyoo 41
zilizojengwa kwa tofali za udongo zimebomoka kuta zake kutokana na mvua
inayoendelea kunyesha mkoani Dodoma katika mtaa wa chinyoya kata ya kilimani
manispaa ya Dodoma huku watu zaidi ya 300 wakiwa wameathirika na mvua hizo.
Akizungumza na kituo
hiki baada ya kuzungukia mtaa huo na kufanya tathmini ya maafa hayo diwani wa
kata hiyo ya kilimani Neema Mwaluko,amesema kutokana na maafa hayo
tayari amewasiliana na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Dodoma mjini na
mbunge wa jimbo hilo na kutoa taarifa juu ya maafa hayo.
Mbunge wa jimbo la
Dodoma mjini Anton Mavunde ametoa msaada wa unga kilo 300 na sukarai kilo 75
huku diwani huyo akiomba watu wengine kuweza kuwasaidia wananchi hao
walioathirika na hali hiyo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa mtaa huo wa chinyoya Faustina Bendela amesema kubomoka kwa nyumba
hizo kunatokana na mtaa wake kutokuwa na mifereji ya kutolea maji na barabara
za kudumu na mtaa huo bado haujapimwa hivyo wananchi kutoshindwa kujenga nyumba
bora na imara .
ukiangalia Dodoma sasa
ni makao makuu ya serikali na huku mtaa wake ukiwa na zaidi ya wananchi 3500
kwa sensa ya mwaka 2012,ambapo mpaka sasa idadi ya watu imeongezeka
kwa wananchi wengi kuhamia katika mtaa huo.
Ikumbukwe kuwa miezi
miwili iliyopita katika zoezi la usafi katika mtaa huo mkuu wa mkoa
wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge,alitoa agizo kwa mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma
kuhakikisha mtaa huo unafanyiwa mpango wa upimaji ili wananchi wa mtaa huo
waweze kujenga ujenzi wa nyumba bora ili kuendana na hadhi ya makao makuu.
Na ANIPHA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment