Mwenyekiti wa shirikisho
la vyama vya waganga wa Tiba asili Mkoa wa Dodoma amewahimiza waganga wa tiba asili kuwaelekeza wagonjwa wa
kifua kikuu katika huduma za afya kupatiwa matibabu bora.
Bwana ISSA MOHAMEND
MDOWE ameyasema hayo wakati akizungumza na Dodoma FM kufuatia agizo
lililotolewa mwishoni mwa wiki na serikali kupitia Waziri wa Afya Mh Ummy
Mwalimu la kuwataka waganga wa Tiba asili kushirikiana na Serikali kuwabaini
wagonjwa wa kifua kikuu.
Amebainisha kuwa
dawa za asili bado hazijafikia kiwango cha kutibu ugonjwa wa kifua kikuu hivyo ni bora
waganga wa tiba asili kuwapatia maelekezo wangojwa hao kuwahi kufika katika
hospitali kwa matibabu zaidi.
Bwana MDOWE amesema
wapo tayari kushirikiana na wizara ya afya kwa kuwatembelea wanachi
vijijni na kuwaelekeza kuhusiana na wagojwa wa kifua
kikuu kwenda hospitali kwa yeyote atakayepata dalili za kuugua kifua kikuu.
Baadhi ya wananchi
wamezungumza na Dodoma FM na kusema kuwa Kutokana na ukosefu wa elimu ya
kutosha juu ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa
Wananchi hasa wa vijijni wamekuwa na imani kuwa ugonjwa huo hautibiki na
kupelekea kubaki nyumbani pasipo kufika hospitali.
Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment